
Chelsea
wako tayari kuongeza dau mpaka kufikia £30m kwa straika Rooney, gazeti
la the Daily Mail limeandika. Ofa ya mwanzo iliyokua £25m ilikataliwa
ila kwa sasa the Blues hawaoni taabu kuongeza mpaka kufikia £30m na
kumlipa Rooney mshahara wa £240,000 kwa-wiki.
Ilhali, the Daily
Star lenyewe limeandika kwamba Rooney meonekana akicheza mchezo wa golf
katika klabu ya gofu iliyopo karibu kabisa na kiwanja cha mazoezi cha
Chelsea(Cobham) - kiwanja ambacho wachezaji wengi wa Chelsea hupenda
kucheza pia. Inamaanisha nini? wewe mwenyewe pigia mstari.
Maoni ya FullSoka: Nionavyo, Rooney kucheza golf katika kiwanja kilicho
karibu na viwanja vya mazoezi vya Chelsea, jambo hilo halina uhusiano
wowote na uwezekano wa jamaa huyo kuhamia Chelsea - nachojua ni kwamba
Jose Mourinho anamtaka sana na Rooney nae anataka sana kuondoka, ila
mzigo upo kwa mchezaji mwenyewe kuiandikia United barua rasmi ya kutaka
kuondoka - ingawa inajulikana United imedaiwa hata kwa hali hiyo
watagoma kumuuza ila nionavyo mimi ikifikia hatua hiyo basi itabidi
wanyanyue mikono na kumuuuza.
Vyanzo - (Daily Mail) & (Daily Star).