Mshambuliaji diego farland ambe kawa sasa anachezea soka katika ligi ya
Japan na klabu ya Cerezo Osaka, amefunguka na kutoa kauli kuhusu mahusiano yake na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez.
Kwa mujibu wa makala ya
Forlan katika jarida 442, amenukuliwa akisema kwamba alimshawishi sana
Suarez kujiunga na Manchester United na sio Liverpool wakati Mruguay
mwenzie alipokuwa Ajax 2011.
Forlan aliandika:
Tuna ukaribu na
tunaelewana sana. Ni mpole na mstaarabu na anapenda kujifunza, mara zote
huniuliza maswali na ushauri. Wakati Liverpool walipotoa ofa kwa ajili
yake, nilimshauri aende Manchester United, lakini pia niliiongelea kwa
uzuri Liverpool na historia yao. Nilimwambia namna nilivyofunga goli la
kuwatoa Liverpool kwenye Europa League nikiwa na Atletico , mashabiki
wao walinishangili baada ya mchezo.
Anapenda kuichezea
Liverpool. Anaipenda Premier League – na mashabiki wanampenda kwasababu
ni mshambuliaji na mchezaji mzuri kiujumla."
Pia Forlan akasema kama angeambiwa amchagua mchezaji bora wa EPL msimu huu basi ingekuwa ngumu kumchagua Kun Aguero au Suarez.
Home
Unlabelled
DIEO FORLAN:NILIMSHAURU LUIS SUAREZ JIUNGE NA MANCHERSTER UNITED
DIEO FORLAN:NILIMSHAURU LUIS SUAREZ JIUNGE NA MANCHERSTER UNITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment