Mansoor Yusuf Himid Ashikiliwa na Jeshi la Polisi

Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia na kumhoji aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe Samaki (CCM) Mansoor Yussuf Himid baada ya kupatikana na silaha ya shortgun yenye risasi 112, bastola na risasi 295 huku wakishikilia laptop yake.
Polisi walifika nyumbani kwa Mansoor asubuhi na kupekuwa na kugundua vitu hivyo baada ya kupata taarifa kwa wasamaria wema kuonesha wasiwasi wao kwa Mansoor.
Naibu Msaidizi Mkuu wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi aliwaambia waandishi wa habari kwamba pamoja na umiliki wa silaha hizo upo kisheria lakini anapaswa kuwa na risasi za shortgun 50 ambapo risasi za bastola kisheria anatakiwa awe nazo 25 kwa Tanzania Bara na Zanzibar.
Risasi 5 zimetumika na polisi wanafuatilia zimetumika vipi.

No comments:

Post a Comment

Subscribe

Flickr