ASP na Muungano

Ishara za uwazi ni kwamba wakati wa 1964 utawala ulijiendesha kwa misingi ya serikali tatu. Kama yuko wa kupinga basi aje na hoja ili tuelimishane pale ambapo pana utata. Ukitazama msingi mzima wa utawala wa wakati ule wa post revolution ni nguvu za vyama na maamuzi yote makubwa na mdogo huwa na roots kutoka katika vyama viliongoza kwa bara na visiwani.
Nguvu za ASP ziliongezeka maradufu baada ya mapinduzi na hata ukitazama zile controversial issue zote zilizotokea wakati wa post revolution japo mataifa makubwa duniani na tasisi za haki za binaadamu kama amnesty international zilisukuma zaidi malalamiko kwa serikali ya muungano, ukweli ni kwamba serikali ya muungano haikuwa na nguvu kubwa kushurtisha Uongozi wa ASP na ndio maana yaliendelea.
Hata vitu viliongoza agenda ya mabadiliko na discipline ya maisha kwa wananchi kama ndio reforms kubwa za mwalimu hazikuweza kuwa na effect zanzibar. Kwa mfano uhasishwaji wa azimio la arusha zanzibar halikufika na kwa wanaotueleza mzee karume alisema siasa za kwao na zetu tafauti. Ukitazama kwa undani japo mfumo wa serikali mbili ulikuwa umesimikiwa ndani ya nchi tayari lakini upande wa zanzibar ukijitegemea na kujiendesha opposite kabisa na politics za kijamaa zilizotawazwa rasmi bara chini ya uongozi wa mwalimu. ASP iliongoza serikali ya zanzibar na ikajitwisha maamuzi yake yakawa ndio maamuzi ya serikali ya zanzibar.
Kwa upande wa bara, ni TANU iliojiongoza chini ya misingi ya ujamaa na kuweka mikakati yake ya maendeleo under policies za ujamaa na kujitegemea na hata kiongozi mzee karume hakuwa na interference kwa maamuzi ya mwalimu yaliohusu masuala ya bara kwa jumla yasiokuwa ya muungano na kubwa lililokuwa zuri kwa mzee karume na ASP kwa jumla katika muungano ni aggressive policies za muungano katika masuala ya defence ambayo zanzibar ilinufaika nayo kama vile bara walivyonufaika na sentiments za ukombozi kwa waafrika na usimikwaji kwa serikali ya kiafrika yenye ulinzi madhubuti.

Nathubutu kusema kwamba kama si muungano serikali ya ASP sifikirii kama ingeliweza kubakia madarakani kwa vile tayari Hizbu party ilikwisha anza kampeni za kuomba msada wa kurejesha serikali yake kupitia kwa nchi walizoshirikiana nazo kama egypt na kwa mwalimu kuruhusu urejeaji wa serikali zenye aliance kubwa na nchi za kiarabu ilikuwa ngumu kwake kumeza na pia ingelikuwa ngumu kwake kwani tayari nyufa za umoja zilikwisha anza kuimega TANU hasa kwa yale magurupu ya waislamu waliokuwa tayari kutokuwa na masikilizano mazuri naye. Tazama namna gani jaribio la mapinduzi wakati wa utawala wa mwalimu na namna gani alisaidiwa na uingereza kurejesha discipline katika jeshi na namna alivyowaadhibu aliowatuhumu kushiriki katika majaribio yale, jee unafikiri suala la kuinunganisha bara na zanzibar lilikuwa kwa best interest ya ASP pekee? Hakufaidika kwa kuwa na nguvu za kuzuia mabadiliko ndani ya volatile zanzibar iliokuwa na influence pamoja na powerful enemies wa mwalimu aliokuwa akiwaita mabeberu?
Kwa upande wa ASP hawakuwa na khofu ya kumezwa kwa wakati ule kwa vile at the end the buck ends na msimamo wa ASP hasa ukizingatia siasa za wakati ule. Demokrasia kwa wakati ule na uchanga wake hususan barani afrika uliegemezwa zaidi na nguvu za chama, na ndio maana mzee karume katika matamshi yake alitueleza kwamba asingeruhusu vyama mpaka baada ya miaka hamsini na ndio sababu za kuwaingiza makoredi na baadhi ya wafuasi wa ZNP ambao walifanana katika misingi ya ujenzi wa nchi mpya. Hakukuwa na lolote ambalo serikali ya muungano ingeliweza kulifanya kwa zanzibar bila ya consent ya chama kwanza na ndio maana zanzibar hatukujuwa nini hasa azimio la arusha na zile strategies za vijiji vya ujamaa rekodi zinaonyesha mzee karume na serikali ya ASP ilipinga.
Nimeyaeleza haya kuonyesha buffer iliokuwapo wakati ule katika uendeshwaji wa serikali ya muungano. Wale ambao walikuwa na intellectual influence hasa katika gurupu la makomred, ASP waliwapeleka kwa serikali ya mwalimu kwa vile kuwepo kwao zanzibar ilikuwa ni threat kwa integrity ya chama chao. Hii inaonyesha kwamba ASP ilijaribu kufanya majaribio ya suluhu lakini kwa mgongo wa kuwapa madaraka wenye nguvu hasa za kielimu kwa upande wa muungano kwa madhumuni mawili makubwa, kwanza ni kujinusuru na influence zao katika siasa za zanzibar, na pili kujilinda na attempt zozote za annexation ya muungano kwa kutumia hila na ghilba za kisomi ambazo zingekuwa ngumu kwao kuzibaini mapema. Angalia kwa mfano, ukimsikiliza katibu wa BLM wakati ule anasema wakati wa mazungumzo ya muungano aliambiwa akanyowe ndevu, na hata justice Dorado hakushirikishwa katika uasisi wake na baada ya kurudi zanzibar mabishano yaliozuka tunaambiwa mzee karume ndie aliesema atamrudishia mwenyewe Mwalimu karatasi zake ikiwa BLM halijawafik. Ukichungulia kwa undani zaidi wapingaji walioongoza wakati ule ni wazee wa Umma party na wale waliokuwa na muono mkubwa wa kielimu. Kwa ASP muungano uliwapa afuweni ya strong defence, ndani na nje, na kwa mwalimu alikuwa na legal base ya kuhakikisha zanzibar inabakia kuwa na influence ya utawala wa kiafrika ambao pia ni safe zone kwa utawala wake.
Kwa misingi hii utakuwa mfumo wa muungano ulianza kwa principles za serikali tatu, under the umbrella za vyama vyenye kushika hatamu ya mwisho ya uongozi. Zanzibar kukiwa na ASP na bara kukiwa na TANU. Na muungano ukifanywa orientation ya makubaliano baina ya ASP na TANU sio maamuzi ya moja kwa moja ya rais wa muungano pekee. La kujiuliza kwa nini ASP na TANU havikuungana mapema kama ni kweli kulikuwa na azma ya kweli kabisa hasa upande wa zanzibar wa kuunganisha nchi mbili kuwa moja?
Natoa mfano wa Sinn Fein kama chama kikongwe ndani ya Ireland chenye lengo la kuirejesha Ireland katika republic moja. Urahisi wa chama hichi ndani ya pande zote mbili za North na south ni kwamba agenda imeanza kwa kuweka serikali moja katika nchi moja. Mashirikiano yao kwa sasa katika Northern Ireland katika serikali ya umoja wa kitaifa ni kuhakikisha matarajio yao yanafanyika through diplomacy na attributes za kweli za democracy. Kinachoonekana hapa ni kwamba ni rahisi wakati wa struggle za independence kwa vyama vyenye malengo yanayofanana kuungana ikiwa lengo ni kuunda serikali moja ya taifa moja. Contrary to muungano wa zanzibar na tanganyika vyama havikuungana japo vikisumiliwa kwamba vikiwa karibu na hata tukielezwa kwamba mapinduzi yenyewe yalifanyika kwa msaada mkubwa wa wanajeshi kutoka bara chini ya uhuru wa serikali ya TANU.
Kwa nini baada tu ya mapinduzi vyama havikuungana lakini ikawa serikali? Hivi ni kweli kwa msingi huu tutaweza kusema kwamba sababu madhubuti ya muungano ni umamjumui wa kiafrika (pan africansim)? Ikiwa ni umajumui wa kiafrika kwa jinsi ya TANU na ASP zilivyoshirikiana na lengo hasa kuunda serikali moja basi ingelikuwa rahisi zaidi kwa kuungana kwa vyama vyenyewe kwanza kuliko serikali. Hii inaonyesha azma tafauti baina ya waasisi, na ndio maana kwa upande wa zanzibar suluhisho bora kwa ASP ni muungano wa serikali ila nguvu zote za kimaamuzi zikabakia katika ngazi za vyama husika. Jee huu ni mfumo wa serikali ngapi kama si tatu, ya ASP, TANU na ya best interest ya pande mbili ie ya muungano?
Wapi palipoanzia hizo kero za muungano? Ni baada ya executive power moja kuanza strategies za kufanya maamuzi bila ya ushirikishwaji wa pande ya pili. Yaani ni attempts ndogno ndogo za kuhalalisha muungano wa serikali moja na ndio hapo palipoanza nyufa za kutofahamiana baina ya pande mbili chini ya uongozi wa ASP na uhai wa mzee Karume. Ushahidi ni hotuba zake na kubwa linalopewa refernce kubwa ni quatation ya muungano kama koti. Hivi ni kweli kauli hii ni muasisi alietamani serikali moja?
Zanzibar nhawakuungana kupoteza nchi yao, walichokubali ni ku-delegate baadhi ya mamlaka yao kwa upnade wa pili kwa sababu za kiusalama zaidi, maingiliano ya muda mrefu ya kidugu, ujirani pamoja na maendeleo ya pamoja. Kosa kubwa la wapemda muungano wa sasa ni kudharau tanko la kusema zanzibar si nchi. Kutoweza kutafautisha status za mamlaka na nchi ndio zilizohamasisha anti union sentiments na kuwa chanzo cha haya tunayoyaona sasa. Msingi mkuu wa mfumo huu wa sasa ulijengwa na buffer ya uongozi wa utatu kwa misingi ya ASP kwa upande wa zanzibar na TANU kwa upande wa bara, hivyo hakukuwa na changamoto kubwa za tanganyika wakati ule kuvaa joho la muungano kwa vile utafauti wa uongozi ulibainishwa kwa tafauti za vyama vinavyoongoza baina ya pande mbili vikiwa na nguvu kubwa ya kimaamuzi kushinda hata serikali za ndani na ya muungano. Kupotea kwa buffer hii na kulazimisha serikali moja chini ya uasisi wa chama kimoja ndio uliouwa maazimio ya muungano na hatuwezi kusema ni coincidence kwamba haya yametokezea after kifo cha mzee karume.
Katika era ya Mzee Jumbe, lililofanywa la mwanzo ni fukuza fukuza za MBM wote waliokuwa na mzee karume, lilifanyika kwa awamu. Ukisikiliza masimulizi ya famili za wazee hawa utakuta waliishi kwa udhalili aftermath ya mzee karume na alibakia mmoja aliekuwa na influence kubwa nae ni Mzee Bavuai. Pili kukafanyika uvunjwaji wa buffer ilioasisi muungano katika mfumo wa utatu na kuundwa serikali moja ndani ya pazia katika kiini macho cha mfumo wa serikali mbili. Hapo hakukuwa tena na regard ya assumed article of union na kila jambo likawekwa katika umbrela ya serikali moja na ndio mtetemeko ulipoanza wa kufukuzwa kwa rais wa zanzibar mhe Aboud Jumbe.
Kama ingelikuwa buffer imezingatiwa ya utatu ulio chini ya ASP na TANU hivi kweli Mwalimu angeliweza kumtimua Mzee Jumbe? Hivi kweli mambo ya muungano yangeliweza kuengezeka kutoka machache mpaka yakafika 30 na kuendelea? Kama si uvunjwaji wa buffer ya Utatu kwa asasi ya vyama tafauti tungeliweza kufikia hapa na kero zote zilizojaa?
Mwalimu alifahamu kwamba serikali haikuwa na nguvu yoyote bila ya vyama kuungana, na hivi ni nani vile aliekuja na ushauri wa kuunganisha vyama? Jee unafikiri nyuma ya pazia lengo la kuunganisha vyama lilikuwa ni lipi? Kwa nini mzee karume na wengine hawakufikiria kuunganisha vyama kwanza kabla ya serikali kama kweli lengo ni serikali moja? Tumeshuhudia nguvu zilizowekwa kwa chama ni kuwa zilzidi hata serikali ya zanzibar na kuifanya kuwa under the thumb za chama tena ndani ya vikao hivyo maamuzi yakafanyika bila ya zingatio la thuluthi mbili kwa pande zote huku tukijuwa kabisa kusingelieweza kufanyika lolote bila ya wajumbe wa tanganyika walio wengi kukubali hata kama wazanzibari wote wangelikwenda na azimio tafauti. Case study uchaguzi wa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama tawala 2000, chama kilishika hatamu against wingi wa wajumbe wa wazanzibar na ndio leo hii tunaendelea kupiga kelele za muungano wa serikali mbili wakati ukweli ni pseudo goverment ya chama kimoja kilichoshika hatamu.
Nikubali kitu kimoja, kwamba mheshimiwa Warioba ni mfuasi wa kweli wa siasa za mwalimu, maana katika hili la serikali tatu, kajijenga zaidi katika ufanisi wa serikali na upanuzi wa demokrasia, lakini misingi ya hatamu ya chama bado kaibakiza pale pale kwa kuwa anajuwa nguvu za chama ndio mhimili mkuu wa serikali ya muungano. Alichokileta yeye ni uwazi wa mfumo wa serikali tatu kwa ajili transparency, ufanisi na utatuzi wa kero katika masuala yanayoongozwa na upana wa demokrasia zaidi pamoja na accountability.
Ukweli uasisi wa muungano ulikuwa kwa miaka 13 wa mfumo wa serikali tatu kisiasa na buffer ya utatu ilipoondoshwa kighilba na hadaa ndio zalio la kero, na hata kwa sase giza la kutoonekana kwa article of union pamoja na ratification order kutoka BLM la kuridhia muungano.

No comments:

Post a Comment

Subscribe

Flickr