
FA wamekubali matumizi ya Vanishing Spray, baada ya majadilino na chama cha waamuzi nchini Uingereza ambacho kimeafiki matumizi ya Spray hiyo ambayo mashabiki wengi walianza kuiona wakati wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.

Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini Uingereza FA Richard Scudamore, amesema imewalazimu kupitisha Vanishing Spray, kwa lengo la kupiga hatua ambapo wanaamini malalamiko huenda yakapungua kutoka kwa wachezaji pamoja na mameneja ambao wamekua wakipingana na waamuzi inapotokea adhabu ndogo.
Kutokana na maazimio hayo, Uingereza wanakubali kusudio la pili kutoka shirikisho la soka duniani FIFA la kumaliza utata uwanjani baada ya kufanya hivyo wakati wakipitisha matumizi ya mfumo wa utambuzi wa mpira kuvuka mstari wa goli *Goal Line Tecknology* ambao ulianza kutumika kwenye ligi ya nchini humo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment