1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo.
kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa
kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua
kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri
hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana
maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa
hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya
kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia.
Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo
lazima.
3.
Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo
pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati
mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani
amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea
kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.
4.
Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na
wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo
mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi
kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka
kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna
lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika
tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye
kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.
5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli
hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi
kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri
kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.
6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa
na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo
hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo
ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona
amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au
matendo yako mabaya dhidi yake.
7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama
kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo
fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa
moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe,
anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.
8.
Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo
fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha
pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata
radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza.....
Udakuspecially.
Home
Unlabelled
OGOPA SANA HAYA MANENO KWA MWANAMKE ANAPOYASEMA!!