Wayne
Rooney tayari ametayarishiwa namba ya jezi Chelsea, limeandika gazeti
la the Daily Star. Gazeti limedai kwamba straika huyo wa Manchester
United atatinga namba 23 - yenye hadhi kubwa iliyofanywa maarufu na staa
wa mpira wa kikapu Michael Jordan, kama atajiunga na the Blues.
Ingawaje the Daily Mirror limeripoti kwamba Chelsea wana uhakika
watampata Rooney kabla dirisha la usajili kufungwa na, kama magazeti
mengine yalivyoandika, yakumnukuu Jose Mourinho kusema watu wape
watulivu kuhusu windo lake hilo.
Vyanzo - (Star) & (Mirror).