Dar es Salaam. Shirika lisilo la Kiserikali la Children’s
Dignity Forum (CDF), limebainisha kuwa ongezeko la watu katika miji
mikubwa nchi linachangia wanafunzi wengi kushindwa kumaliza elimu ya
msingi na sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti, alibainisha hayo jana katika uzindizi wa ripoti ya watoto na miji nchini.
Alisema, kutokana na wingi wa watu wanaoishi
mijini na mrundikano wa magari,, watoto wengi wamekuwa wakishindwa
kumaliza elimu kwa sababu hakuna magari ya kuwapeleka shule.
“Katika majiji mengi kumekuwa na wimbi kubwa la
watoto wanaoshindwa kumaliza elimu kwa sababu mbalimbali ikiwa ni
pamopja na kukosekana kwa magari ya kuwapeleka shule,” alisema Mtengeti.
“Katika hili utawakuta vijana wengi wameacha shule
na kuanza kufanya kazi za ndani, ukahaba na hatimaye watoto wenye kati
ya umri wa miaka 10 hadi 18 ndiyo wanaopata maambukizi ya virusi vya
ukimwi,” alisema.
Alibainisha kuwa kutokana na hali hiyo wako katika
mchakato wa kupanga pamoja na manispaa zote za majiji hayo ili
kutengeniza mpango wa pamoja wa kutatua changamoto zinazowakumba watoto
hao.
SOURCE,MWANANCHI
SOURCE,MWANANCHI