Christian
Benitez, ambaye alishawahi kuichezea Birmingham City Premier League,
amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 27 kwa mstuko wa moyo.
Akiwa
anawindwa na Tottenham, straika huyo wa kutegemewa wa taifala Ecuador
alikua amekamilisha uhamisho uliogharimu £10million kuhamia klabu ya
Qatari iitwayo El Jaish akijiunga kutokea klabu ya Mexican iitwayo Club
America wiki chache zilizopita.
Alishiriki mchezo wake wa kwanza
akiitumikia klabu yake hiyo mpya siku ya jumapili dhidi ya Qatar SC, na
baadae alikimbizwa hospitali baada ya mchezo akisumbuliwa na maumivu
makali ya tumbo - na baadae kupatwa na mshtuko wa moyo na kupoteza
maisha.