Bayern Munich iliwafunga wapinzani wao wa Ujerumani Borussia Dortmund 2-1 katika fainali ya mabingwa wa ulaya katika uwanja wa Wembley mwezi Mei, lakini hakuna yoyote katika timu hizo zilizocheza fainali ambayo imeifikia Juventus kimapato.
Mabingwa wa Italia wameingiza kiasi cha €65.3 million kutoka kwenye ligi ya mabingwa msimu uliopita, €10 million zaidi kuliko Bayern Munich.
Dortmund wamefuatia kwa kutengeneza kiasi cha €54.2 million.
Vilabu 32 vilivyoshiriki katika hatua ya makundi vimegawana kiasi cha €904.6 million, kwa mujibu wa Uefa.
Tofauti kubwa iliyopo baina ya miamba iliyocheza fainali na Juve ilikuwa ni haki za matangazo ya TV, kwa wataliano wa Turin wakiingiza kiasi cha €44.8 million kupitia haki za matangazo ya TV, ukilinganisha na €19.1 million walichoingiza Bayern.
AC
Milan, ambao waliweza kuingia raundi ya pili tu, wenyewe waliingiza
kiasi cha €51.4 million mbele ya miamba ya Hispania Real Madrid (48.4m)
na Barcelona (45.5m) miamba ya Ufaransa Paris Saint-Germain (44.7m).
Pamoja na kufanya vibaya kwenye michuano hiyo lakini pia timu za England safari hii zimeshuka sana kwenye kuingiza fedha nyingi - mabingwa wa nchi hiyo Manchester United ndio wamewaongoza wenzao kwa kuingiza €35.6 million.
Timu ambayo imeingiza fedha kidogo kabisa ilikuwa ni Dynamo Zagreb waliingiza kiasi cha €10.5 million.

CHANZO; SHFFIH DAUDA