Mabadiliko: Diamond kutua Dar kesho saa moja asubuhi akitoka Marekani kweye tuzo za AFRIMMA

Diamond Platinumz amelazimika kubadili ratiba ya kutua katika uwanja wa ndege wa mwalimu Julius Nyerere akitokea Marekani alikoenda kuwakilisha Tanzania katika tuzo za AFRIMMA na kushinda tuzo ya mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki. Ambapo mashabiki wake wanatarajiwa kumpokea.
Mkali huyo wa Bongo Flava ameiambia 100.5 Times F kuwa amelazimika kubadili ratiba ya safari yake kutokana na mabadiliko ya ndege aliyopaswa kusafiri nayo, hiyo badala ya kufika leo saa nane usiku kama alivyokuwa ametaarifu awali, atafika kesho saa moja kamili asubuhi.
“Kiukweli Flight yangu ilikuwa inatakiwa iwepo kuanzia siku ya leo saa nne. Lakini bahati mbaya kutokana na matatizo ya ndege kuingiliana huku na kule hatujajua…imebidi connection ziwe nyingi sana. Ilibidi kupelekea kufika kesho kwenye saa moja kama na nusu hivi ndio tutakuwa tunadondoka.
“So, kwanza niombe radhi, najua watu wengi walikuwa wanataka kuja lakini bahati mbaya imekuwa hivyo ni nje ya uwezo wetu. Kama watu wana nguvunguvu naomba tukutane pale saa moja asubuhi mimi ndio nadodondoka.” Amesema Diamond kwenye maelezo yake.

No comments:

Post a Comment

Subscribe

Flickr