Ajira uhamiaji zasitishwa kutokana na kashfa kubwa ya upendeleo

Zoezi la kuajiri wafanyakazi wapya wa kitengo cha Uhamiaji Tanzania limeingia dosari baada ya kukumbwa na kashfa nzito ya wafanyakazi wa ketengo hicho kupeana kazi kwa upendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, nafasi zilizosistishwa ni za Konstebo na Koplo wa uhamiaji.
Kufuatia kashfa hizo nzito ziliozelekezwa kwa maafisa wa Uhamiaji kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari, Katibu Mkuu Abdulwak ameunda kamati maalum ya chunguzi wa tuhuma hizo hali inayowaweka matatani baadhi ya maafisa wa Uhamiaji.

No comments:

Post a Comment

Subscribe

Flickr