Khalid
Mohamed, Top In Dar (T.I.D) ambae pia ni mmiliki wa Top Band amepinga
vikali taarifa zinazoonesha kuwa Nyimbo za msanii mwenzake Ali Kiba
zinasikilizwa zaidi Muscat huenda kuliko msanii mwingine wa Bongo Fleva.
Taarifa hizi zilizotolewa na mtandao wa
Bongo5 ambao ulipata maelezo ya kina baada ya kuchat na mtanzania aishie nchini Muscat aliyetambulika kwa
jina la Rayya Al Habsi aliyewapa tathmini kuhusu nyimbo za kibongo zinazosikilizwa zaidi huko mjini Muscat,Oman.
Rayya
alisema nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa sana lakini pia wasanii
wengine wanaopendwa ni Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na Dully Sykes.
Rayya
aitaja pia upande wa mduara kuwa ni AT, Off side Trick na Kilimanjaro
Band, na kwamba band inayofunika zaidi ni Twanga Pepeta.
Taarifa
hizi zinakuja wakati ambapo T.I.D amepata deal la kwenda mjini Muscat
kupiga show akiwa na band yake ‘Top Band’, na hivyo ameona kama taarifa
hizi zimepotoshwa na yeye ndiye alistahili kutajwa katika nafasi
aliyopewa ‘Ali Kiba.’ Na kwamba yeye ameshapiga show mara mbili na
anaenda kwa mara ya tatu akiwa na band yake.
Kupitia ukurasa wake wa facebook T.I.D a.k.a Mnyama amedondosha maelezo confidently.
“This
came after I have been mentioned perfoming well its too late for this
reminder its my time,and they listen to me alot its my third time
perfomin there and this time with my band.”
Kisha akaambatanisha
na kichwa cha habari chenye picha ya Ali Kiba kama kilivyoandikwa na
Bongo5, yenye kichwa cha habari “Nyimbo za Ali Kiba zinasikilizwa zaidi
Muscat ‘huenda’ kuliko msanii mwingine wa Bongo Flava.”
Well,
yale yanaweza kuwa ni maoni ya Rayya, maoni sio utafiti rasmi japo
unatoa picha ya jumla. Lakini inaonekana kama Top In Dar hataki kuwa
Down any where hivi hivi.
Home
Unlabelled
TID AFUNGUKA BAADA YA KUSIKIA KWAMBA Ali Kiba anasikilzwa zaidi Muscat, asema ni muda wake “It’s too late for this reminder it’s my time”