Mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Rasimu ya Katiba
Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wanachama na viongozi wake.
UTANGULIZI
1.1 Mnamo tarehe 03/06/2013 Tume ya Mabadiliko ya
Katiba ilitangaza rasimu ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mabaraza ya Katiba ya Wilaya, ambayo yameshaundwa
na yatatoa maoni yake kupitia mikutano itakayoitishwa na Tume ya
Marekebisho ya Katiba. Mabaraza haya yanasimamiwa na Tume yenyewe.
Mabaraza ya Asasi, Taasisi na makundi ya watu
wenye malengo yanayofanana kama vile vyama vya siasa na jumuiya za
kidini na kadhalika. Mabaraza haya yanasimamiwa na Asasi au Taasisi
husika.
1.3 Chama Cha Mapinduzi kimeshajiunda kama Baraza
la Katiba la kitaasisi na kutambuliwa rasmi na Tume kwa barua Kumb.na.
AB 76/386/57 ya tarehe 24/052013
1.4 Kwa kuzingatia kwamba Chama Cha Mapinduzi ni
Taasisi muhimu na yenye masilahi makubwa katika upatikanaji wa Katiba
Mpya, Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa iliyokutana mjini Dodoma
Tarehe, 10/6/2013, pamoja na mambo mengine ilielekeza kwamba uandaliwe
utaratibu utakaohusisha utoaji wa maoni utakaotumiwa na wanaCCM kutoa
maoni yao.
1.5 Madhumuni ya ufafanuzi huu ni kujenga uelewa
wa pamoja wa maudhui ya Rasimu ya Kwanza na hivyo kuwawezesha wanaCCM
kushiriki kutoa maoni yao kikamilifu kutoka ngazi ya matawi hadi taifa.
UTARATIBU WA KUTOA MAONI
2.1 Kwa upande wa matawi maoni yatatolewa kupitia mikutano
Kwa wilaya, mikoa na taifa. Maoni yatatolewa kupita halmashauri kuu zao.