Mwigizaji
maarufu Swahiliwood Muhsin Awadhi(Dr. Cheni leo anaadhimisha siku yake
ya kuzaliwa(birthday). Kama kawaida kwa siku muhimu kama hii kwa kila
mtu, watu mbalimbali humtakia mhusika afya njema na maisha marefu,
mafanikio na kila la kheri huku wengine pia wakitoa au kuelezea hisia
zao kwa mlengwa. ElizabethDr. Cheni ndiye aliyemuingiza Lulu katika sanaa kwa kumpeleka Kaole na hata baada ya kukumbwa na matatizo bado yupo bega kwa bega na Lulu. Dr. Cheni ni mmoja wa waigizaji wenye mchango mkubwa katika tasnia ya maigizo na filamu nchini akiwa ametamba na michezo kadhaa kipindi hicho ITV na baadaye katika filamu na kupelekea waigizaji wengi chipukizi kuhamasika kuingia katika sanaa ya filamu. Baadhi ya filamu alizoigiza ni pamoja na Nipende Monalisa, Danger Zone, Majanga, Jessica na nyinginezo.
HAPPY BIRTHDAY Muhsin Awadhi(Dr.Cheni)