NAWAOMBA WANAOWEZA KULIJIBU WAJIBU KWA NJIA YOYOTE ILE AMBAYO MIMI NAWEZA KULIPATA JIBU LAKE....
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
1. KWA
JINA LA RAHMANI MOLA
ULIYETIYA
NIJAZE SIHA MOYONI NIWEZE
KUULIZIYA
SWALI HILI YAKINI NISHACHOKA VUMILIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI
ATANIAMBIYA
2. BATA
ANA SIRI GANI
NANI ATANIAMBIYA
ANIJUZE KWA UNDANI KILA NILOKUSUDIYA
AANZE MWAKE BANANI HADI
ANAPOCHUMIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI
ATANIAMBIYA
3. LENGO
LAKE ASILANI BATA SIJALIGUMIYA
NIMECHUNZA VITABUNI NA PIYA KUULIZIYA
BATA ALIWAZA NINI HADI
NYUMA KUBAKIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI
ATANIAMBIYA
4.
ENGEWAWEKA PEMBENI KAMA
ANAWAHOFIYA
WAKIPITA MITAANI WATAKUJA KUPOTEYA
WATAKUWA SALIMINI MOTE WATAMO CHEZEYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
5. BATA
AFANYA UHUNI WATOTO
KUFUATIYA
JAMANI BATA KWANINI YEYE NYUMA HUBAKIYA
BATA ALIWAZA NINI NIMEHOKA FIKIRIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
6. HAPA
KUNA KUBWA SHANI TUNAWEZA
JIVUNIYA
UCHUNGUZI TUFANYENI NA AKILI KUTUMIYA
OMI SIFANYI UTANI HAYA
NINAYO WAMBIYA
7.TANGU
MWAKE UTOTONI BATA MAJI HUCHEZEYA
SIJUWI BATA KWANINI KARONI HUPENDELEYA
TENA BATA KISIRANI USIKU HUUCHEZEYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
8. KAMA
NITAWATAJENI KAZI ITANIZIDIYA
KILA ALIYE MAKINI JIBU
NALISUBIRIYA
ANIJUZE REDIONI AU
SIMO TAPOKEYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
9. JAMANI
NAWAOMBENI HARAKA KUNIJIBIYA
ILI NIWE FURAHANI MOYO
UPATE TULIYA
BATA JAMANI KWANINI YEYE NYUMA HUBAKIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
10.HAPA
NAFIKA MWISHONI TUNGO IMEKAMILIYA
ALO BINGWA REDIONI AJIBU SAWA SAWIYA
ZAWADI IPO NJIYANI MWENYEWE
TAFURAHIYA
BATA ANA SIRI GANI NANI ATANIAMBIYA
MTUNZI,MTOTO OMARI KHAMISI OMARI(OMMTOBYY)
MARKAZ
KIZIMBANIWETE-PEMBA
CHINI YA MWALIMU WANGU BINGWA MAPENGO
NO,0773 593545