MGANGA
Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dk Ezekiel Mpuya amesema tangazo
lililotolewa hospitalini hapo la kuwataka watu kuvaa mavazi ya heshima
wanapoingia hospitalini hapo lilikuwa likihusu
watumishi wa hospitali hiyo na si wananchi wa kawaida.
Akizungumzia
suala hilo juzi, Dk Mpuya alisema kuwa Katibu wa Hospitali hiyo alitoa
tangazo hilo kimakosa hali ambayo ilisababisha walinzi kuzuia watu
waliovaa ‘ovyo’ kuingia hospitalini hapo.
“Uongozi
wa Hospitali unaomba radhi kwa usumbufu waliopata wagonjwa na wananchi
waliofika hospitalini hapo kwani tangazo lilitolewa kimakosa na Katibu
kwani lilikuwa likiwahusu watumishi pekee na si wananchi,” alisema Dk
Mpuya.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, Hospitali
ya Mkoa wa Dodoma iliweka masharti ya uvaaji ambapo mavazi yaliyopigwa
marufuku ni sketi fupi, fulana zisizo na mikono nguo za kubana pamoja na
Jeans.
Juzi
kulitokea kutoelewana kati ya walinzi na watu waliokuwa wakitaka
kuingia hospitalini hapo na kuzuiwa kutokana na aina ya mavazi
waliyokuwa wamevaa.
mpekuzihuru
Home
Unlabelled
WAVAA VIMINI WAPIGWA MARAFUKU KUINGIA HOSPITALI YA MKOA WA DODOMA.